Russia yadaiwa kupeleka wanafunzi wa kiafrika kupigana vita Ukraine - Bloomberg
Eric Buyanza
June 10, 2024
Share :
Urusi inadaiwa kutuma maelfu ya wahamiaji na wanafunzi wa kiafrika kupigana katika vita vyake dhidi ya Ukraine kwa ahadi ya kuwaongezea muda wa visa huku ikiwatishia kuwafukuza nchini humo wale wanaokataa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg, tathmini iliyofanywa na baadhi ya maafisa wa Ulaya na kuja na ripoti yao, Urusi imekuwa ikitishia kutorefusha visa za wanafunzi wa Kiafrika na wahamiaji wengine vijana isipokuwa kama watakubali kujiunga na jeshi la nchi hiyo.
Urusi pia imekuwa ikiwasajili wafungwa kutoka kwenye magereza yake.
Inaelezwa kuwa baadhi ya waafrika nchini humo walio na visa za kazi huzuiliwa na kulazimishwa kuamua kati ya kufukuzwa au kupigana, afisa mmoja wa Ulaya alisema.
Chanzo: BLOOMBERG