Ruto ajitetea kuodi ndege kwenda Marekani, Wakenya wamjia juu
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Rais wa Kenya William Ruto kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) amekanusha madai ya kutumia gharama kubwa kwenda kwenye ziara Marekani kwa kukodi ndege binafsi.
Rais Ruto ameandika hayo leo Jumapili Mei 26, 2024 huku akidai gharama ingekuwa kubwa zaidi kama angetumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).
“Wakenya wenzangu, nimeona wasiwasi wenu kuhusu njia yangu ya usafiri hadi Marekani. Kama msimamizi anayewajibika wa rasilimali za umma na kulingana na azimio langu la kuishi kulingana na uwezo wetu, napaswa kuongoza kwa kuwa mstari wa mbele, gharama ilikuwa ndogo kuliko kusafiri kwa KQ.”
Mapema wiki iliyopita Rais Ruto alifanya ziara nchini Marekani na alikaribishwa na mwenyeji wake Rais Joe Biden.