Ruto amuunga Mkono Raila Urais AU
Sisti Herman
July 30, 2024
Share :
Rais wa Kenya William Ruto siku ya jana Jumatatu Julai 29, ameunga mkono wasilisho la nchi hiyo ambapo wamewasilisha rasmi Mgombea wa mpinzani wa kihistoria, Raila Odinga, kumrithi Moussa Faki Mahamat wa Chad, katika kinyang’anyiro cha urais wa Umoja wa Afrika. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 2025.
Kenya bado inabidi kuyashawishi Mataifa ya Afrika kumpigia kura mgombea wake ambapo tayari imepata uungwaji mkono kadhaa, kama vile Uganda, Zimbabwe na Algeria. Nchi nyingine kadhaa katika ukanda huo kama vile Djibouti, Somalia na Ushelisheli zikiwa zimetangaza kuwania nafasi hiyo.