Ruto atangaza mawaziri 11 kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri
Eric Buyanza
July 19, 2024
Share :
Rais William Ruto ametangaza mawaziri kumi na moja kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri.
Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Ruto amesema idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa wiki ijayo.
Ruto amesema uteuzi huo ambao pia umemjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali umekuja baada ya mashauriano ya kurudisha amani na utulivu katika nchi hiyo.
Orodha hiyo pia iko na Mawaziri sita waliofukuzwa kazi awali, ambao sasa wanarejea katika wizara tofauti, huku Prof. Kithure Kindiki na Adan Duale pekee wakiendelea kushikilia nafasi zao za awali.