pmbet

Ruud Van Nistelrooy kurejea Manchester United

Eric Buyanza

June 25, 2024
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy, anaweza kurejea Manchester United kama sehemu ya wakufunzi wa Erik ten Hag huko Old Trafford.

Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 47 anaweza kuchukua nafasi ya msaidizi wa Ten Hag, Mitchell van der Gaag au kocha wa mbele Benni McCarthy, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi.

Van Nistelrooy aliichezea United kati ya 2001 na 2006, akifunga mabao 150 katika mechi 219 chini ya Sir Alex Ferguson.

Hata hivyo bado kuna ukakasi kweye mpango huo, kwani Van Nistelrooy pia yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Burnley ili kuchukua nafasi ya ukocha iliyoachwa na Vincent Kompany aliyejiunga na Bayern Munich mwezi uliopita.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet