Rwanda yapokea wakimbizi wanaotaka hifadhi kutoka Libya
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Rwanda imepokea wakimbizi 90 na wanaotafuta hifadhi kutoka Libya chini ya mpango unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR).
Wakimbizi hao na wanaotafuta hifadhi walihamishwa chini ya mpango wa Dharura ambao umeshuhudia wakimbizi 2,150 wakitumwa Rwanda kutoka Libya tangu 2019.
Kwa mujibu wa RFI, Kuwasili kwa wakimbizi hao kunakuja wakati Uingereza ikijaribu kupitisha sheria mpya ambayo itaruhusu nchi hiyo kutuma Rwanda baadhi ya wakimbizi wanaoomba hifadhi.
Mahakama ya Juu ya Uingereza hapo awali ilibatilisha mpango huo na kusema unakwenda kinyume cha sheria.