pmbet

Rwanda yataka malipo kwa mchango wake wa usalama Msumbiji

Eric Buyanza

April 17, 2026
Share :

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuondoa wanajeshi wake kuanzia Mei kutoka jimbo lenye mgogoro la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji ambako Rwanda imekuwa kwenye operesheni ya kupambana na wanamgambo waasi wa kiislam.
 

Kwa kufanya hivyo inaelezwa kuwa anauweka Umoja wa Ulaya chini ya shinikizo kubwa kama hautatoa ahadi ya kutoa ufadhili wa uhakika.
 

Umoja wa Ulaya umechangia Euro milioni 40, ambazo inadaiwa ni moja ya tano ya gharama zote za Rwanda inazotumia.

 

Tangu mwaka 2021, wanajeshi wa Rwanda wamekuwa wakilinda eneo hilo kwa ombi la serikali ya Msumbiji.
 

NI GHARAMA GANI HASA ZA OPERESHENI YA KIJESHI YA RWANDA?
 

Kiwango halisi cha gharama hizo bado kinabishaniwa. Mtaalamu wa usalama kutoka Msumbiji, Borges Nhamirre wa taasisi ya utafiti wa usalama, anaeleza katika mahojiano na DW kuwa takwimu zilizowasilishwa na Kigali ni vigumu kuthibitishwa.

 

Rwanda, kwa mfano, huhesabu gharama za usafiri kupitia shirika la ndege la serikali RwandAir—lakini "hakuna anayejua kama gharama hizo zilitokea kwa kiwango hicho.” Inawezekana hivyo kuwa gharama zote zimeonyeshwa kuwa kubwa zaidi kuliko zilivyo kwa kweli, anasema mtaalamu huyo anayefuatilia hali ya usalama Cabo Delgado.

 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet