S2kizzy: Msijifanye hamuoni, 'Komasava' ina-hit dunia nzima
Sisti Herman
June 11, 2024
Share :
Mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, S2kizzy amefunguka kwamba ingawa watu hawazungumzii sana kuhusu wimbo wa msanii Diamond Plutnumz ambao yeye ameshiriki kuutayarisha “Komasava”, ila ndio moja ya nyimbo kubwa zaidi duniani kwa sasa.
Challenge ya wimbo huo ambao Diamond ameashirikisha wasanii wawili maarufu wa mziki wa 'Amapiano' kutoka nchini Afrika Kusini Chley na Khalil Harrison imechezwa sana kutoka kwa watu wa mataifa mbalimbali Ulimwenguni.