S2kizzy na Abbah kwenye vita kali mtandaoni
Sisti Herman
May 3, 2024
Share :
Waandaji (Producers) maarufu wa muziki nchini S2Kizzy na Abbah wameingia kwenye vita ya meneno kwenye mitandao ya kijamii kila mmoja akijitamba kuwa bora zaidi ya wengine na kutotaka kufananishwa na mwingine.
S2kizzy aliandika kupitia Insta Story yake kuwa "Msinifananishe na producer mwingine yeyote Afrika Mashariki, mimi ni bora kwenye kizazi hichi"
Abbah naye akaandika "Nina mwaka sasa sijaingia studio kugonga mdundo lakini mtaa unaimba Abbaaah, ni heshima kiasi gani kwenye kizazi changu, wakinyamaza naleta mdundo mwingine mpya waendelee kujifunza"
Je unadhani kati ya hao nani mkali?