Sababu za Diddy kutoshtakiwa kisheria hizi hapa
Sisti Herman
May 19, 2024
Share :
Baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha Diddy akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie huku baadhi ya watu wakitaka rapa huyo ashitakiwe, Mwanasheria wa Wilaya ya Las Angeles , DA George Gascón ameweka wazi kuwa Diddy hawezi kushitakiwa kwa video hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya mwanasheria huyo sababu kuu inayomfanya Diddy asishitakiwe ni kuwa tukio limeshapita muda wake. Kama ilivyoripotiwa awali, tukio husika lilitokea Machi 5, 2016, katika Hoteli ya ‘InterContinental’ hivyo hawakuweza kuwasilisha mashitaka kwa sababu ya muda kupita.
Hata hivyo taarifa hiyo ilidai kuwa ni ngumu kufananisha tabia ya mtu aliyokuwa nayo mwaka 2016 na sasa na endapo tabia hiyo ingetokea mara nyingi basi Diddy angeweza kushitakiwa.
“Kufikia leo, watekelezaji wa sheria hawajawasilisha kesi inayohusiana na shambulio lililoonyeshwa kwenye video dhidi ya Bw. Combs, lakini tunahimiza mtu yeyote ambaye amefanyiwa ukatili au anaushahidi wa hivi karibuni atoe taarifa kwa vyombo vya sheria au kuwasiliana na Ofisi yetu ya Huduma za Waathiriwa,” DA George Gascón alisema.
Sheria ya California kwa wahanga wa shambulio lolote wanatakiwa kufungua mashitaka muda wa shambulio au miaka mwaka mmoja kupita hivyo basi, kulingana na ratiba ya tukio, hakuna mashitaka yanayoweza kufanya Diddy akamatwe.