pmbet

Sadio Mané amwaga Bilioni 55 kwenye kilimo cha maembe kijijini kwao

Eric Buyanza

September 22, 2026
Share :

Nyota wa soka wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Al-Nassr, Sadio Mané, amezindua rasmi mradi mkubwa wa kilimo na usindikaji wa maembe ujulikanao kama "SM10 Agro" kijiji kwao Bambali.
 

Uwekezaji huo unagharimu faranga bilioni 11.7 za CFA, ambazo ni sawa na takribani dola milioni 20.4 za Kimarekani au zaidi ya shilingi Bilioni 55.6 za Kitanzania.

 

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich aliweka jiwe la msingi la mradi huo mnamo tarehe 19 Septemba 2026, akilenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii katika ukanda wa Sédhiou.

 

Kulingana na mpango wa mradi huo, SM10 Agro inatarajiwa kutengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya 1,000 wakati wa uzinduzi, huku kukiwa na fursa ya kuongezeka hadi ajira 2,500 kadri uzalishaji unavyopanuka.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sadio Mané alieleza kusikitishwa kwake na ukweli kwamba ukanda wa Sédhiou hupoteza kati ya 30% hadi 40% ya maembe yanayovunwa kutokana na ukosefu wa viwanda na maghala bora ya kuhifadhia mazao.
 

"Nataka utajiri wetu ubaki kwetu. Faida za mradi huu zinapaswa kuwasaidia na kuwanufaisha watu wetu," alisema Mané.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet