Safari ya kwenda Urusi, ATCL yaanza kwa kishindo na abiria 242
Eric Buyanza
July 6, 2026
Share :

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeanza kwa kishindo safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Moscow kupitia Zanzibar baada ya ndege yake aina ya Boeing 7878 Dreamliner kurejea alfajiri ya jana ikiwa na zaidi ya abiria na watalii 242.
Akizungumza katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Zanzibar, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema idadi hiyo ya abiria ni ishara kuwa safari hizo zimeanza vizuri.
“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake haya. Julai 2 tulisafiri na ndege hii kwenda Moscow kuzindua safari za moja kwa moja kati ya Moscow na Dar es Salaam kupitia Zanzibar.
Leo tumerejea na watalii na abiria zaidi ya 242. Huu ni ushindi,” alisema. Alisema serikali itaendelea kuboresha huduma za usafiri wa anga na miundombinu mingine ya usafiri ili kuongeza tija kwa sekta ya utalii na uchumi wa nchi.
TSN





