"Safari yangu ya kubadilisha jinsia imeenda vizuri" - Bobrisky
Eric Buyanza
March 22, 2024
Share :
Shoga maarufu wa nchini Nigeria, Bobrisky ambaye amebadilisha jinsia kutoka mwanaume na kuwa mwanamke, anasema safari hiyo ya kubadilisha jinsia ili kuwa 'mwanamke kamili' ilienda vizuri.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, alitupia picha yake akionekana mwenye furaha na mabadiliko hayo aliyoyafanya, huku akisema hakupata changamoto yoyote ya kiafya wakati wa upasuaji.
Bobrisky akawashukuru wahudumu wa afya wa Nigeria na wale wa nje ya nchi kwa usaidizi wao katika kurahisisha mabadiliko yake ya kuwa mwanamke.
"Safari yangu ya kubadilika kuwa mwanamke imeenda vizuri, hakuna changamoto za kiafya nilizopata, kila kitu kimekwenda sawa"
"Ninataka kusema asante kwa madaktari wangu wa nyumbani na nje ya nchi. Nyote mmefanya kazi ya kutukuka kwenye mwili wangu,” aliandika.