Safari za treni zasitishwa na shirika
Sisti Herman
January 18, 2024
Share :
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa limesitisha kwa muda huduma ya safari
za treni kutoka Dares Salaam kuelekea Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga na Mwanza, pamoja na Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli katika maeneo ya Mazimbu, Kilosa na Munisagara Mkoani Morogoro, Godegode na Gulwe Mkoani Dodoma pamoja na maeneo ya Ruvu junction, Wami, Mvave Mkoani Pwani, pia eneo la Mkalamo Tanga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua
zinazoendelea na huduma ya usafiri wa treni zinatarajia kuanza siku ya Jumanne January 23, 2024 katika reli ya kati na kuelekea Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro a Arusha) inatarajiwa kuanza January 29, 2024 baada ya kukamilika uimarishaji wa miundombinu ya reli.
“TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inawasihi Wananchi kuwa wavumilivu katika
kipindi cha matengenezo ili kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama”