Saha; Old Trafford inatia aibu
Sisti Herman
May 17, 2024
Share :
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Louis Saha amedai kuwa viongozi wa klabu hiyo wanawakosea heshima mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mazingira mabaya ya uwanja wa Old Traffords ambayo yamefikia hali yakuaibisha kutokana na uchakavu wa samani hadi kufikia hali ya paa kuvuja wakati wa mvua.
"Nimemsikia Gary Neville akilalamika kuhusu hilo mara nyingi, na amekuwa akiionya klabu kuhusu hilo kwa muda. Ili kufikia hatua hiyo, ilikuwa ni aibu sana.
"Viongozi wanapaswa kuwajibika kwenye hili mashabiki wanalipia tiketi kwahiyo wanahitajika kupata huduma nzuri wanapokuja kufuata burudani ya timu yao.
Alisema mchezaji huyo wa zamani ambaye kwasasa ni mchambuzi wa vipindi vya michezo.