Saidi ajinyonga hadi kufa baada ya kunyimwa kuchungulia simu ya mkewe
Eric Buyanza
April 25, 2024
Share :
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Said Mziray mkazi wa Kata ya Muriet Jijini Arusha amejinyonga kwa mtandio na kupoteza maisha April 22 mwaka huu chanzo kikisadikika kuwa ni kunyimwa simu ya mkononi na mke wake ili kutazama alikuwa anachati na nani?
Baada ya mke kumnyima simu kulitokea ugomvi mkubwa baina yao hadi kupelekea mwanamke huyo kuondoka nyumbani na kurudi kwa wazazi wake.
Tangu kutokea kwa ugomvi huo Said alianza kutishia kujiua hadi ilipofika Jumatatu alipoamua kutimiza adhma hiyo.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 ameacha mke mmoja na watoto wadogo wa tatu.
Angalia video hapo chini;