Saido na Aziz Ki kukutana leo kufuzu AFCON 2025
Sisti Herman
October 13, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya Burundi leo watakuwa wenyeji wa timu ya Taifa ya Burkina Faso katika mechi ya marudiano ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON mwaka ujao.
Mechi iliyopita Intamba Murugamba, walipata kipigo kutoka kwa Burkina Faso cha mabao 4-1, Burundi wakiwa wa kwanza kuliona lango.
Nahodha wa Burundi Saido Ntibazonkiza na mchezaji wa Yanga Stephanie Aziz Ki leo watakutana dimbani kwenye mtanange wa leo baada ya Saido kukosekana katika mchezo uliopita.
Burundi inahitaji alama tatu muhimu katika mchezo wa leo ambao utapigwa majira ya saa moja za usiku nchini Ivory Coast katika mchezo ambao kocha Etienne NDAYIRAGIJE ataingia akiwa na presha kubwa.