Saido ndo basi tena Simba
Sisti Herman
June 19, 2024
Share :
Saido Ntibazonkiza amemaliza mkataba wake Simba SC na leo rasmi Simba wametangaza kuwa hatokuwa sehemu ya kikosi chao kwa msimu ujao.
Saido anaondoka Simba akiwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa misimu miwili mfululizo
2022/23 - magoli 17
2023/24 - magoli 11
Saido Ntibazonkiza amehusika katika mabao mengi (60 + ) zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika NBC Premier League tangu msimu wa 2020/21.