pmbet

Sajil 2, Kombora hatari la Iran linalofika Israel kwa dakika 7

Eric Buyanza

June 27, 2025
Share :

Sajil ni kombora la balistiki la masafa ya kati lenye uwezo wa kufikia maeneo lengwa hadi kilomita 2,000. Kwa masafa haya, kombora hili linaweza kulenga Mashariki yote ya Kati, ikiwemo Israel, kusini mashariki mwa Ulaya, na sehemu za Asia ya Kati, likirushwa kutoka Iran. Ikiwa litarushwa kutoka mji wa Natanz nchini Iran, linaweza kufika jiji la Tel Aviv nchini Israel kwa dakika saba tu. 

Kombora la Sajil lina urefu wa takriban mita 18 linatumia mafuta imara, jambo linalolipa faida dhidi ya makombora yanayotumia aina nyingine za mafuta ya kawaida. 

Kutokana na matumizi yake ya mafuta imara, linaweza kuandaliwa kurushwa haraka zaidi, lina uwezo bora wa kuhifadhi vilipuzi, na linaweza kuwa na ufanisi zaidi wakati wa mapigano.

Kombora hili linaweza kubeba kichwa cha kivita chenye uzito wa takriban kilo 700, kwa mantiki hiyo lina uwezo mkubwa wa uharibifu dhidi ya maeneo lengwa. Jaribio la kwanza la mafanikio la kombora hili lilifanyika mwaka 2008 na katika jaribio hilo lilifunika umbali wa kilomita 800. Jaribio lake la pili lilifanyika Mei 2009, likijaribu teknolojia ya hali ya juu na mifumo ya ulipuaji.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimkakati na Mafunzo ya Kimataifa (Center for Strategic and International Studies), "Kunaweza kuwa na aina kadhaa za kombora la Sajil. Mwaka 2009, Iran ilijaribu kombora lililoitwa Sajil 2. 

Ripoti isiyothibitishwa inasema kwamba Sajil 3 inaweza kuwa bora zaidi. Sajil 3 ni kombora la hatua tatu lenye masafa ya juu ya kilomita 4,000 na uzito wa kilo 38,000."
Iran haijajaribu kombora la Sajil hadharani tangu mwaka 2012, lakini lilijaribiwa wakati wa mazoezi ya kijeshi mwaka 2021. 

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet