Saka awasaidia wahanga wa tetemeko Morocco
Sisti Herman
December 21, 2023
Share :
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya England Bukayo Saka, ametoa vyumba 50 vya kontena kusaidia walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Morocco, liliotokea Septemba mwaka huu na kusababisha watu zaidi ya 2800 kupoteza uhai na maelfu kujeruhiwa.
Msaada huo aliotoa akishirikiana na shirika la kutoa misaada la ‘BigShoe’, ambao nao wametoa makazi kwa watu 255, wakiwemo watoto 89.