Saka na Odegaard kuikosa Sunderland leo.
Joyce Shedrack
February 7, 2026
Share :
Arsenal wanatarajia kuwakosa Bukayo Saka na Martin Odegaard watakapomenyana na Sunderland katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza leo.
The Gunners kwa mara nyingine tena wako pointi sita mbele kilele cha msimamo wa Ligi ya soka Uingereza na huku washindani wao Aston Villa na Manchester City wakiwa ugenini dhidi ya Bournemouth na Liverpool wikendi hii, pengo hilo linaweza kuongezeka tena.
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hakuwa na Saka wala Odegaard wakati washika mitutu hao wakijikatia tiketi ya fainali ya Kombe la Carabao kwa ushindi dhidi ya Chelsea Jumanne usiku.
Nafasi zao leo kikosini zitashikwa na Noni Madueke na Eberechi Eze.





