pmbet

Sakata la Manchester City lamuibua Pep Guardiola.

Joyce Shedrack

September 30, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Manchester City Pep Guardiola ameandika ujumbe wake wa kwanza baada ya klabu hiyo kukutwa na hatia ya makosa 114 kati ya 115 yaliyohusishwa na kanuni za kifedha za ligi ya Uingereza.

Pep Guardiola breaks silence on Man City verdict after club found guilty of  serious financial breaches

Guardiola ameandika ujumbe wake kuonyesha mshikamano na klabu, akiwataka mashabiki wa City duniani kote kujua kwamba bado yuko pamoja nao.

 

“Nataka kila shabiki wa Manchester City duniani ajue kwamba niko hapa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.”

Akaongeza kuwa ataendelea kuwa nyuma ya klabu, mmiliki, mwenyekiti, Ferran Soriano, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki.

 

“Niko pamoja nanyi kila wakati, na nitakuwa pamoja nanyi niko wazi tutapitia hili pamoja.”

 

Ujumbe huo umefika siku moja baada ya Tume Huru ya ligi ya Uingereza kutangaza uamuzi wake kuhusu ukiukaji wa kanuni za kifedha wa City katika kipindi cha 2009/10 hadi 2017/18. 

 

Manchester City imekanusha makosa hayo na imetangaza nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kabla ya hukumu rasmi kutoka.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet