Salah ashauriwa kutokwenda kucheza Ligi ya Marekani
Eric Buyanza
March 30, 2026
Share :

Mkurugenzi wa timu ya taifa ya Misri, Ibrahim Hassan, amemtahadharisha Mohamed Salah juu ya kujiunga na Major League Soccer (MLS) baada ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu, akisema kuwa hatapata umaarufu mkubwa kama aliopata.
Hassan alisema kuwa Salah anapaswa kubaki Ulaya kwakuwa ana ofa kutoka Paris Saint-Germain, Bayern Munich, na vilabu vya Ligi ya Italia.
Aliongeza kuwa kama Salah hatapata ofa kutoka Ulaya, basi kujiunga na Ligi ya Saudi Arabia itakuwa chaguo zuri, hasa kwa kuwepo kwa nyota kama Cristiano Ronaldo.
Hassan alisema kuwa kujiunga na MLS kutamfanya Salah asiwepo kwenye kurasa za vyombo vya habari, ukilinganisha na Lionel Messi ambaye alijiunga na Inter Miami mwaka 2023.
Salah, ambaye ana miaka 33, bado hajamua kuhusu mustakbali wake baada ya kuondoka Liverpool, ambapo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Uingereza na Ligi ya Mabingwa.





