Salah kutocheza dhidi ya Sudan Kusini kwasababu ya uwanja wa nyasi bandia
Sisti Herman
September 27, 2026
Share :

Mohamed Salah hatasafiri na kikosi cha Misri kwenda Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wenye nyasi bandia, Shirikisho la Soka la Misri (EFA) lilisema Jumamosi.
''Kulikuwa na makubaliano kati ya benchi la ufundi la timu ya taifa na Mohamed Salah kabla ya mchezo dhidi ya Angola kwamba hatacheza dhidi ya Sudan Kusini, na benchi la ufundi lilipendelea utaratibu huu ili kumlinda mchezaji huyo," EFA iliongeza.





