Salah na De Bruyne walikua watoto chelsea - Mourinho
Sisti Herman
December 19, 2023
Share :
Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kuwauza mastaa wa wanaotamba sasa kwenye Ligi Kuu England, Kevin De Bruyne na Mohamed Salah nyakati zake akiwa Chelsea , akisisitiza kuwa walikuwa wadogo sana kipindi hicho, na walikuwa na tamaa ya mafanikio.
“Kusema kweli, walitaka kuondoka kwa sababu walionyesha nia wenyewe, hawakutaka kusubiri mafanikio kwa muda mrefu, historia inaonyesha uamuzi wao ulikuwa na maana kubwa sana, kuna wakati watoto wanafanya uamuzi wa haraka sana, wakati mwingine maisha yao ya soka yanaenda kwa njia tofauti, hawakuwa wavumilivu au kusubiria muda muafaka.” alisema Mourinho kwenye mahojiano na Podcast ya Mikel Obi ambaye pia amewahi kuwa mchezaji wa Chelsea.
Kocha huyo akiwa Chelsea alimuuza De Bruyne kwenda klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani na Salah AS Roma amabyo anaifundisha sasa baada ya kukosa nafasi ya kuanza Chelsea. Tangu mastaa hao walipoondoka Chelsea, wameimarika maradufu na kuwa wachezaji bora wa Ligi Kuu England, huku mashabiki wakimponda Mourinho sababu ya uamuzi wake wa kuwauza kipindi hicho.