pmbet

Salah ndo basi tena Afcon

Sisti Herman

January 21, 2024
Share :

Shirikisho la soka nchini Misri limesema kuwa baada ya kumfanyia uchunguzi nyota wa klabu ya Liverpool na Captain wa timu hiyo limegunduwa kuwa alikazwa na msuli kwenye mchezo wao dhidi ya Ghana.

 

Salah alifanyiwa mabadiliko kwenye kipindi cha kwanza kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 2-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Ghana kwenye fainali za mataifa ya Afrika Alhamis iliyopita.

 

Mohamed Salah ataikosa michezo miwili inayofuata ya Misri, mchezo wa kwanza ni ule wa mwisho wa kundi B na mwingine kama timu hiyo itafuzu hatua ya 16 bora.

 

Waraka wa timu ya Taifa ya Misri umesema “Vipimo vya X-ray ambavyo amefanyiwa nahodha wa Misri Mohamed Salah vinaonyesha kuwa alikazwa na msuri ya nyuma ya mguu”.

 

“Hivyo atakosa michezo miwili ijayo ya fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde lakini pia mchezo wa hatua ya 16 bora kama timu itafuzu hatua hiyo”.

 

Kama Misri haitafuzu hatua ya 16 bora basi Salah atakuwa amecheza michezo miwili pekee katika fainali za mataifa ya Afrika, akifanya hivyo dhidi ya Msumbiji na Ghana ambayo hakumaliza.

 

Hadi hivi sasa kundi B ni Cape Verde pekee ambayo imefuzu kwenda hatua ya 16 bora ya fainali za mataifa ya Afrika ambayo imefikisha alama sita baada ya kuifunga Ghana na Msumbiji.

 

Misri ipo nafasi ya pili ikiwa na alama mbili [2], Ghana ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama moja [1] na msumbiji ipo nafasi ya nne ikiwa na alama moja [1].

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet