pmbet

Salum jela miaka 30, kisa kila 15 za bangi!

Eric Buyanza

February 13, 2024
Share :

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Namkongo, Tarafa ya Nangaru, Salum Dadi (41) kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki kilo 14.8 za dawa ya kulevya aina ya bangi.
 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Maria Batraine baada ya kuridhishwa pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa umewasilishwa mbele ya mahakama hiyo.
 

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea, akiiomba mahakama isimpe adhabu kali kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza, ana familia wakiwamo watoto wawili, mke na wazazi wanaomtegemea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet