Samatta afunguka ugomvi na kocha Stars
Sisti Herman
January 18, 2024
Share :
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars Mbwana Samatta amezungumza baada ya
mchezo wa kwanza wa Taifa Stars kwenye mashindano ya Afcon2023 yanayoendelea Nchini
Ivory Coast mchezo waliocheza dhidi ya Timu ya Morocco na Taifa stars kupoteza mchezo huo
kwa idadi ya magoli 3-0.
Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta
amezungumza na vyombo vya Habari na kusema kambi ya Taifa stars ipo sawa na hakuna
mgawanyiko wowote katika kikosi hicho kilichopo Ivory Coast.
Hata hivyo,kulikuwa na maswali mengi kuhusu nahodha Samatta na kocha mkuu wa Taifa stars
Adel Amrouche ya kwanini hawakupeana mkono wakati Samatta akifanyiwa mabadiliko kwenye
mchezo huo huku wengine wakihisi pengine wana ugomvi, Samatta ameondoa sintofahamu
hiyo akikiri kuwa hana ugomvi na kocha.
Akizungumzia mchezo huo Samatta amesema Morocco walikuwa bora zaidi yao lakini
wameyapokea matokeo na wanajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Zambia ili kupata matokeo
mazuri.