Samatta na Job waachwa Taifa Stars
Sisti Herman
March 13, 2024
Share :
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Suleman "Morocco" ameita kikosi cha wachezaji 23 kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya FIFA Series 2024 ambapo Tanzania itacheza michezo miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Mongolia na Bulgaria kuanzia tarehe 22-24.
Kwenye kikosi hicho chenye wachezaji 23, wachezaji 10 wanacheza klabu za ligi za nje ya Tanzania, 13 wanacheza klabu za ligi ya ndani ambapo klabu ya Yanga imcehangia wachezaji watano, Simba wachezaji wanne na Azam wachezaji wanne.
Gumzo kubwa baada ya kutajwa kikosi hicho ni kuachwa kwa nahodha wa timu ya Taifa Tanzania Mbwana Samatta na beki wa Yanga Dickson Job.
Hichi hapa kikosi kinachoingia kambini;
GOLIKIPA.
Aishi Manula [Simba]
Aboutwaleeb Mshery [Yanga]
Kwesi Kawawa [Syrianska, Sweden]
WALINZI
Bakari Mwamnyeto [Yanga]
Ibrahim Hamad [Yanga]
Lusajo Mwaikenda [Azam]
Haji Mnoga [Aldershot Town, England]
Mohamed Hussein [Simba].
Novatus Dismas [Shakhtar Donetsk, Ukraine]
Kennedy Juma [Simba].
Miano Danilo [Villena, Hispania]
VIUNGO.
Feisal Salum [Azam]
Mudathir Yahya [Yanga].
Morice Michael [RFK, Novi Sad, Serbia]
Himid Mao [Tala’ea El Geish, Misri]
Yahya Zayd [Azam]
Tarryn Allarakhia [Wealdstone, England].
WASHAMBULIAJI.
Clement Mzize [Yanga]
Saimon Msuva [Al Najma, Saudi Arabia]
Kibu Denis [Simba]
Abdul Suleiman [Azam]
Ben Starkie [llkeston Town, England]
Charles Mmombwa [Macarthur, Australia].