pmbet

Samia anafanya kazi nzuri, lazima tumsifu - Kinana

Eric Buyanza

December 13, 2023
Share :

Akiwa kwenye Mkutano wa wananchi wa Jimbo la Chato mkoani Geita jana, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurhaman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi nzuri na ndio maana watu wanamsifu.
 

“Lazima tukubaliane Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi… kuongoza ni kuonesha njia, ukiwa na kiongozi mzuri, msikivu, mwenye kushirikiana na wenzako wakapanga mambo yakawa kwa nini tusimsifu, lazima tumsifu maana ndio anatuongoza, ” amesema Kinana.
 

“Ukimwambia Mkuu wa Mkoa hapa (Martine Shigela) asimame aeleze fedha zilizoletwa katika Mkoa huu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, basi nina hakika fedha zinazotolewa kipindi cha Rais Samia inaweza kuwa mara 10.

“Nilikuwa Kagera wamepewa fedha Sh bilioni 260, nilikuwa Rukwa wamepewa Sh bilioni 256 Mkuu wa Mkoa Geita, ananiambia zaidi ya Sh bilioni 300 zimeletwa kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet