Sancho aanza na asisti Dortmund ikishinda
Sisti Herman
January 15, 2024
Share :
Baada ya kuwa na wakati mgumu katika maisha yake ya soka aliyekuwa winga wa ManchesterUnited JadonSancho ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo BorussiaDortmund ameanza kuonesha makali yake uwanjani.
Ambapo siku ya Jana klabu yake ya Dortmund ilikuwa kibaruani ikicheza na Darmstadt Sancho alifanikiwa kutoa asisti na kifanikisha timu yake kufunga bao la pili.
Mchezo huo ulitamatika kwa mabao 3-0 huku Dortmund ikiondoka na alama zote tatu, Sancho aliingia dakika ya 55 akichukuwa nafasi ya Jamie Bynoe-Gittens na kutoa asisti dakika ya 77.