Sancho ahusishwa kujiunga na Palmerias
Sisti Herman
September 4, 2026
Share :

Jadon Sancho anatazamiwa kuwa mchezaji mpya wa Palmeiras ya Brazil baada ya makubaliano ya awali kukamilika na mchezaji huyo raia wa Uingereza anaweza kuelekea Brazil kujiunga na timu hiyo.
Sancho anatazamiwa kusaini mkataba wa misimu miwili pamoja na chaguo la kuongeza msimu mmoja zaidi baada ya kukosa timu kubwa barani Ulaya.
Jadon Sancho atasafiri usiku huu kutoka London kwenda São Paulo kwa ndege ya LATAM Airlines, huku akiwa anatarajiwa kuwasili alfajiri.
Mara tu atakapowasili, atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake na Palmeiras.
Chanzo: Alfonso Partidor





