Sancho kama Ronaldo kwa Ten Hag - Rio Ferdinand
Sisti Herman
April 17, 2024
Share :
Gwiji wa soka wa Manchester United Rio Ferdinand ambaye kwasasa ni mchambuzi wa vipindi vya michezo amesema kuwa aliyekuwa winga wa Manchester United ambaye kwasasa anakiwasha vilivyo Borrusia Dortumnd Jadon Sancho ameonyesha wazi kile kinachodhaniwa na watu kuhusu uwezo mdogo wa kocha wa Manchester United kuhusiana na mahusiano na wachezaji.
"Sancho, kama ilivyokuwa kwa Ronaldo na wengine anaendelea kutuonyesha kuwa Ten Hag ana walakini kwenye namna ya kuhusiana na wachezaji"
"Kuna namna ya kutatua mapungufu ya mchezaji na siyo kutaja kama vile kwenye vyombo vya habari, wachezaji wote walioondoka kwa mgogoro na yeye hivi sasa wanafanya vyema kuliko timu yake" alisema hivyo Rio.
Rio amesema hayo baada ya kiwango bora cha sasa cha Sancho ambaye ameisaidia Dortmubd kufuzu nusu fainali ya Uefa akilinganisha na mafanikio ya Ronaldo baada ya kuondoka United huku Uited chini ya Ten Hag ikiwa kwenye hali mbaya zaidi.