pmbet

Sancho kutimkia Italia

Sisti Herman

August 15, 2025
Share :

 

Winga wa Manchester United, Jadon Sancho anatajwa kuwa mbioni kukamilisha dili la kutua AS Roma kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Imeelezwa kuwa gharama za dili hilo ni Euro milioni 20 ambapo Roma wanaamini Manchester United watashawishika na dau hilo.

Sancho amekuwa katika wakati mgumu tangu ajiunge na Manchester United na mara kadhaa amekuwa akitolewa kwa mkopo ili kurejesha makali yake lakini bado imekuwa ngumu kupenya kwenye kikosi cha Manchester United.

Hatahivyo inatajwa kuwa mahusiano kati ya United na Sancho yalivunjika muda mrefu tangu enzi za kocha Erik Ten Hag kilichosalia kwasasa ni kuheshimu mkataba baina yao.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet