Sankara Karamoko anukia Jangwani
Eric Buyanza
December 6, 2023
Share :
Klabu ya Yanga inahusishwa kuihitaji saini ya mshambuliaji machachari wa Asec Mimosas, Sankara Karamoko raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 20 kwenye dirisha dogo la uhamisho na usajili la mwezi Januari.
Karamoko msimu huu kwenye ligi ya mabingwa Afrika amefunga bao 1, akipika 1 kwenye wastani wa dakika 20 tu kwenye mechi 2 alizocheza.
Yanga ipo kwenye mchakato wa kuziba nafasi ya mshambuliaji wao hatari aliyeondoka dirisha kubwa lililopita Fiston Mayele, pengo ambalo mshambuliaji raia wa Ghana Hafidh Konkoni ameshindwa kuliziba.