pmbet

Sarah Alex, Bondia namba 1 Tanzania uzito wa Bantam

Sisti Herman

June 12, 2025
Share :

 

Ushindi wake dhidi ya Zulfa Iddy kwenye usiku wa #PMBetNgumiKitaa mwanzoni mwa mwezi June, Bondia Sarah Alex amendelea kujisimika ufalme kwenye orodha rasmi ya Mabondia wanaoongoza nchini Tanzania kwenye uzito wa Bantam.



Hii ni 5 bora ya msimamo wa ubora kwenye orodha rasmi ya mtandao wa kukusanya, kutunza na kuhifadhi takwimu za mapambano ya Mabondia kwa uzito wa Bantam, kuanzia uzito wa kilo 51 hadi 54, kwa Mabondia wa kike Tanzania;

1. Sarah Alex 
2. Tatiana Ezekiel
3. Egine Kayange
4. Dorothea Muhoza
5. Lulu Kayage


Sarah mwenye umri wa miaka 26 anaongoza msimamo huo wa Ubora baada ya kurekodiwa kuwa takwimu hizi;

- Mapambano 8
- Ushindi mara 6
- Sare mara 1
- Kupoteza mara 1
- Raundi 46

Bondia huyo anayepigana 'style' ya orthodox anashika nafasi ya 88 duniani kati ya mabondia 271 wa uzito wake.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet