Saratani ya matiti, usipowahi huathiri mapafu na ini
Sisti Herman
January 29, 2024
Share :
Daktari na mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Lydia Chiguma amebainisha kuwa ni vyema wanawake wakawa wanapima mara kwa mara afya zao ili kujua mapema na kuwahi matibabu ya saratani ikiwemo ya matiti ambayo kama mgonjwa atachelewa inaweza kusambaa na kuathiri maeneo mengine ya mwili kama Ini na mapafu.
"Saratani ukitofautisha na magonjwa mengine huwa ina tabia ya kutoka eneo la chanzo kwenda kwenye maeneo mengine. Mtu anaweza kuwa na saratani ya matiti lakini kwa sababu amechelewa kuanza matibabu huo ugonjwa ukasogea ngazi nyingine kama vile mapafu au ini na kumfanya mgonjwa kuwa na tatizo la ini na mapafu vyote havifanyi kazi ipasavyo." alisema Dkt. Lydia kwenye mahojiano na Jambo Tanzania ya TBC.