pmbet

Sasa Itakuaje ?...!Mama Dangote amuambukiza Uncle Shamte Maradhi.

Joyce Shedrack

July 18, 2024
Share :

Mume wa Mama Dangote mama mzazi wa msanii wa bongofleva Diamond Platnumz amefunguka  kuwa mwanamama huyo amempa maradhi  baada ya  vipimo kutoka.

Uncle Shamte ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram ulioambatana na picha ya Mama Dangote unaosemeka kama ifuatavyo…

Majibu ya vipimo vyote vinaonesha ya kwamba MARADHI yangu ni wewe tu.

1) Mganga kanishauri niwe nakunywa kikombe kimoja cha mate yako kila asubuhi.....

2) Kasema kila mtu ninayeongea naye LAZIMA nikutaje wewe mara 400 ata kama mada haihusiani...

3) Wadudu wa upendo wamezidi kwenye kichwa changu ndo maana nywele zimepotea....

4) Ili mapigo ya moyo wangu yaende sawa niwe nakupa 99 elfu kila kwenye laki 1 ninayoipata....

 Uncle Shamte amemaliza kuandika kwa neno NAKUPENDA ❤️ aliloandika kwa herufi kubwa akithibitisha na kuweka wazi hisia zake juu ya mama mzazi wa staa wa bongofleva nchini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet