Sasa kuvuta sigara hadharani marufuku
Eric Buyanza
April 30, 2024
Share :
Akiongea Bungeni mjini Dodoma leo Aprili 30, 2024, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa Sigara hadharani.
Dkt Mollel amesema hayo wakati akijibu swali namba 215 kutoka kwa Mbunge wa Tumbe, Mhe. Amour Khamis Mbarouk aliyeuliza Je, ni lini serikali italeta Sheria ya Kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani?
Sheria hiyo pia imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha.