pmbet

Sasa Rwanda kukagua mapato ya makanisa

Eric Buyanza

March 13, 2025
Share :

Makanisa na nyumba za ibada 600 zimefutwa kabisa nchini Rwanda huku serikali ikitoa kanuni mpya zinazoratibu uendeshaji wa makanisa na nyumba za ibada. 

Kanuni hizi pia zinasema kwamba ili mtu aruhusiwe kufungua nyumba ya ibada au kanisa, atatakiwa kulipa pesa milioni mbili faranga za Rwanda ambazo ni sawa na dola za Marekani elfu moja na mia sita.

Pia kwa mujibu wa kanuni hizi mpya mtu atakayefungua kanisa au nyumba ya ibada atatakiwa kuwa na elimu ngazi ya Chuo Kikuu katika masomo ya theolojia au mafunzo ya dini.

Lakini kama hilo halitoshi nyumba ya ibada au kanisa itatakiwa kuonyesha mfumo mzima wa uongozi wake na wajibu wa kila mtu lakini pia kuonyesha jinsi mapato yanavyoingia kanisani.

Zaidi lakini huyu atakayehitaji kufungua kanisa au nyumba ya ibada atatakiwa kuonyesha ramani ya jengo la ibada kuhakikisha ikiwa kweli linakidhi viwango vya kuitwa nyumba ya ibada au kanisa.

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet