pmbet

Sativa asimulia Polisi alivyotekwa Dar kupelekwa Arusha na kutupwa Katavi

Eric Buyanza

June 27, 2024
Share :

Kufuatia tukio la kijana maarufu mitandaoni Edger Edson Mwakabela "Sativa", ambaye alitoweka tangu Jumapili June 23,2024 maeneo ya Mbezi kwa Msuguli Jijini Dar es salaam, na kupatikana leo akiwa amejeruhiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani limethibitisha kufanya mahojiano naye huku akisimulia namna alivyochukuliwa jijini Dar es salaam na watu wasiojulikana hadi kupatikana kwake.
 

Akihojiwa na Jamii Forum kuhusiana na tukio Kamanda huyo amesema "Ndio ni kweli, taarifa za tukio hilo lipo na tayari tumeshaenda eneo la tukio na Mgonjwa sasa hivi yupo Hospitali ya Wilaya ya Mlele anaendelea na Matibabu
 

SACP Ngonyani amesema Uchunguzi wa awali umebaini Sativa aliokotwa na Wasamaria wema Usiku wa Kuamkia Juni 27, 2024 Barabarani maeneo ya Pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi (Barabara ya Mpimbwe Majimoto inayoelekea Mpanda)
 

"Mgonjwa ameongea mwenyewe japo kwa shida amesema alikamatwa na watu asiowajua Juni 23 Mbezi kwa msuguli, kisha akapelekwa Arusha katika sehemu asiyoijua na baadae kuletwa Katavi" alisema Kamanda.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet