pmbet

Sauzi yafufua matumaini Afcon

Sisti Herman

January 22, 2024
Share :

Timu ya Taifa ya Afrika Kusini imefufua matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora kuelekea mchezo wa mwisho wa makundi baada ya kupata matokeo matokeo mazuri kwa mara ya kwanza kwenye AFCON 2023 kufuatia ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Wababe wa Tunisia, Namibia.

 

Magoli ya Bafana Bafana yaliyowapa alama 3 muhimu dhidi ya majirani zao yalifungwa na mshambuliaji wa Alhy Percy Tau, na viungo wawili wasjambuliaji wa Mamelod Sundowns Themba Zwane aliyefunga mawili na Thapelo Maseko.

 

Baada ya ushindi huo Bafana Bafana wanasogea hadi nafasi ya 2 kwenye msimamo wa kundi E wakiwa na alama 3, alama moja nyuma ya Mali, wakifuatiwa na Namibia wenye alama 3 pia lakini wametofautiana idadi magoli na Bafana Bafana huku Tunisia wakiburuza mkia na alama 1.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet