pmbet

Schlotterbeck nje ya kombe la dunia baada ya kupata jeraha

Eric Buyanza

June 23, 2026
Share :

Beki wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, ameondolewa rasmi kwenye michuano ya Kombe la Dunia kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.
 

Schlotterbeck alipata jeraha hilo la mishipa ya kifundo cha mguu wakati wa mechi na Ivory Coast ambapo Ujerumani ilipata ushindi wa mabao 2–1 katika mchezo uliochezwa Jumamosi mjini Toronto.

 

Mchezaji huyo wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 26 alilazimika kutolewa kipindi cha mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Antonio Rudiger.
 

Kocha mkuu wa Ujerumani, Julian Nagelsmann, ameelezea kushangazwa vipi mchezaji huyo aliweza kuendelea kucheza hadi mapumziko licha ya jeraha hilo.
 

Schlotterbeck anatarajiwa kubaki nchini Marekani pamoja na wenzake, lakini hatacheza kwa miezi kadhaa ijayo kutokana na majeraha hayo.
 

Kabla ya kuumia, alikuwa ameanza michezo yote miwili ya awali na hata kufunga bao katika ushindi mkubwa wa mabao 7–1 dhidi ya Curacao kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi E tarehe 14 Juni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet