Schweinsteiger: Man United ni timu kubwa kuliko Bayern Munich
Sisti Herman
March 4, 2026
Share :

Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger, ambaye alipata fursa ya kipekee ya kuchezea klabu za Bayern Munich na Manchester United, ametoa mtazamo wake kuhusu ukubwa wa miamba hiyo miwili ya Ulaya.
Licha ya kuwa na historia ndefu na Bayern, Schweinsteiger aliweka wazi kuhusu ushawishi wa klabu hiyo ya Uingereza duniani kote.
Alieleza, “Bila shaka Manchester United ndiyo klabu kubwa zaidi duniani... United inajulikana na kupendwa zaidi kote duniani. Kuna utofauti; Bayern Munich ni klabu kubwa, lakini Manchester United ni kubwa zaidi.”
Kauli yake inasisitiza nguvu ya mashabiki na jina la "Mashetani Wekundu" kimataifa, hata inapovilinganishwa na miamba hiyo ya soka la Ujerumani.





