Scouting Report; Gadiel Michael Debut Match Analysis
Sisti Herman
February 19, 2024
Share :
Aliyekuwa beki wa kushoto wa klabu kubwa za Tanzania Yanga, Simba na Azam aliyejiunga na Cape town Spurs ya Afrika kusini kutokea Singida FG, Gadiel Michael amecheza mchezo wake wa kwanza kwenye DSTV Premier league dhidi ya Amazulu.
Hii ni ripoti fupi ya mchezo wa Kwanza wa Gadiel akiwa na Spurs, wakishinda 3-1, ripoti itaelezea;
- Namna alivyotumika kimbinu
- Takwimu zake kwenye mchezo
MBINU
Gadiel alipangwa kama beki wa kushoto kwenye kikosi cha Ernest Middendorp kwenye mfumo wa 5-4-1 ambao ulinyumbulika kwenye miundo tofauti na kumpa Gadiel majukumu tofauti;
Kuzuia
Spurs wakizuia walitumia mfumo wa 5-4-1, ambao ulimhitaji Gadiel kuwa kwenye mstari wa wachezaji watano mwisho wa uzuiaji.
- Gadiel alizuia mashambulizi ya Amazulu yanayopita kwenye mapana ya uwanja, nyakati nyingi timu yake ilizuia kwenye theluthi mbili za nyuma (mid&low block)
- Hivyo walikaribisha sana mashambulizi ya Amazulu waliokuwa Wakishambulia na muundo wa 2-3-4-1, huku wakitumia wachezaji wawili kwenye mapana ya uwanja mara zote.
- Gadiel alizuia Mchezaji wa Amazulu anayecheza kwenye mapana ya uwanja upande wa kulia(kushoto kwa Spurs) asiweze kuvuka na Kutengeneza nafasi, hasa za krosi.
- Pia kuna nyakati Spurs walizuia kwa kuwafuata Amazulu kwao, jukumu lake likawa ku-track movement za Wing-back huyo wa Amazulu
Kushambulia
Spurs Wakishambulia muundo wao ulibadilika kwenye miundo tofauti ambayo pia ulinyumbulisha majukumu ya Gadiel, kama;
• 3-4-3
- Spurs walitumia muundo huu waliutumia (build up & middle third) nyakati za kujenga na kuendeleza shambulizi
- Hapa akawa na jukumu la kupokea na kuendeleza shambulizi kwenye njia za pembeni, kwenye theluthi ya kwanza na ya kati ya timu yake
• 3-2-5
- Spurs walitumia muundo huu kwenye theluthi mbili za mwisho (middle & final third) kwaajili ya shambulizi kupenya kuta za Amazulu na Kutengeneza nafasi za kufunga
- Gadiel alicheza kwenye mapana ya uwanja upande wa kushoto ili kuendeleza shambulizi au kushawishi kutanuka kwa Kuta za Amazulu kwenda pembeni ili shambulizi la Spurs lipenye Katikati
- Lakini kwenye theluthi ya mwisho Gadiel alikua na jukumu ya kusaidia utengenezaji wa nafasi kutokea upande wa kushoto
TAKWIMU
Takwimu zake kwenye mchezo huo aliocheza dakika 90 zilikuwa;
Kushambulia
- Kugusa mpira - 44
- Pasi - 22
- Pasi ndefu - 5
- Krosi - 2
- Shuti - 1
- Faulo alozochezewa - 2
- Ufanisi kwa ujumla 68%
Kuzuia
- Kutelezea na Kupokonya mpira 3
- Kusafisha (clearance) 1
- Faulo alizocheza 1
- Mipira ya juu aliyoshinda - 2 kati 2
- Mipira ya chini aliyoshinda - 4 kati 6