Sean Diddy apunguziwa wiki 5 za kukaa gerezani.
Joyce Shedrack
March 5, 2026
Share :
Msanii maarufu wa Marekani Sean “Diddy” Combs ameripotiwa kupunguziwa muda wa kifungo chake gerezani. Awali alikuwa anatarajiwa kuachiliwa tarehe 4 Juni 2028, lakini sasa tarehe mpya ya kuachiwa imehamishwa hadi 25 Aprili 2028.
Diddy anatumikia kifungo cha miezi 50 jela kufuatia kupatikana na hatia katika mashtaka yanayohusiana na ukahaba (prostitution-related charges).
Kupunguzwa kwa muda huo kunatajwa kuhusishwa na utaratibu wa mfumo wa magereza nchini Marekani unaoruhusu wafungwa kupata punguzo la muda kutokana na mambo kama tabia njema gerezani na alama za “good time credits.”.





