Seedorf: Mainoo anafanana uchezaji na mimi
Sisti Herman
June 11, 2024
Share :
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa AC Milan, Real Madrid na timu ya Taifa ya Uholanzi Clerence Seedorf amesema kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United Kobe Mainoo anafanana miondoko ya uchezaji na kama alivyokuwa kipindi bado anakichafua dimbani.
Seedorf ambaye baada ya kustaafu soka aliibukia kwenye ukocha akiifundisha AC Milan kwasasa ni mchambuzi mwalikwa kwenye televisheni mbalimbali na aliyasema hayo kwenye moja kati ya tathmini zake kuhusu kinda huyo.
Kauli hiyo ya Seedorf inaenda sambamba na kauli aliyowahi kuitoa mkongwe wa Mnachester United Rio Ferdinand siku za nyuma kuwa Mainoo anafanana staili ya uchezaji na Seedorf.