Selemani Mwalimu aanza safari kwenda Wydad
Sisti Herman
February 4, 2025
Share :
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Suleiman Mwalimu ameanza safari yake ya kuelekea nchini Morocco kujiunga na Klabu yake Mpya ya Wydad Casablanca.
Mwalimu mwenye umri wa miaka 19 amesaini Mkataba wa miaka 4 kuitumikia Wyadad Casablanca itakayo kwenda kushiriki klabu Bingwa ya Dunia nchini Marekani Mwaka huu.
Mwalimu anakua mchezaji wa pili kuchezea Wyadad na mchezaji 5 kucheza ligi ya nchini Morocco.