Selemani Mwalimu amtoa mafichoni Ahmed Ally
Eric Buyanza
August 11, 2026
Share :

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameibuka baada ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Selemani Mwalimu kujiunga na Yanga.
Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho nyota huyo amekwenda kujiunga na wapinzani wao.
“ Wengi tumeingia kwenye taharuki baada ya kuona aliyekuwa mshambuliaji wetu kutambulishwa klabu nyingine. Taharuki kubwa zaidi inatokana na sisi kumtambulisha Mchezaji husika kwenye siku yetu tukufu Simba Day.
“ Kwanza niwape pole Wana Simba kwa taharuki hii Sipo hapa kujielezea nini kimetokea, Kitu muhimu zaidi kwa sasa tuwekeze nguvu kwenye mchezo wetu wa kesho wa Ngao ya Jamii. Hakuna tunachokihitaji zaidi ya ushindi, kwa misimu miwili tumeikosa Ngao ya Jamii.
“ Huu ndio wakati sahihi wa kuchukua Taji hili Insha Allah Akili yetu, fikra zetu, mawazo yetu na nguvu zetu tuzielekeze Amaan Stadium, Safari hii tunatakiwa kuufungua msimu kwa Ubingwa wa Ngao.
“ Tumerithishwa kuipenda Simba yetu hivyo tuendelee kuipigania kesho tupate furaha ya wote. Let's go Wana Simba, Punje ya mchele ikidondoka wali utaliwa tu” alisema Ahmed.





