Selemani Mwalimu kuokoa jahazi leo Tanzania U-23.
Joyce Shedrack
October 6, 2026
Share :
Mshambuliaji Selemani Mwalimu ameongezwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu AFCON utakaopigwa leo.

Mwalimu anaunga na Chuga Boy ambaye aliongezwa pia kwenye kikosi hicho kitakachocheza dhidi ya Kenya.
Tanzania U-23 inahitaji kupindua matokeo ya mabao 4-1 saa 10 jioni katika uwanja wa Uhuru ili kusonga mbele.





